Home Uncategorized MTIBWA SUGAR YAPANIA KUFANYA MAKUBWA 2020/21

MTIBWA SUGAR YAPANIA KUFANYA MAKUBWA 2020/21


 THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa wana imani ya kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21 kutokana na maandalizi yao kuwa makini.


Akizungumza na Saleh Jembe, Kifaru amesema kuwa wana kikosi kizuri chenye wachezaji bora ambao wamesajiliwa ndani ya kikosi hicho chenye ngome yake mkoani Morogoro kwenye mashamba ya miwa.


“Tupo imara kwa msimu huu wa 2020/21 na kila kitu kinakwenda sawa, ukitazama namna ambavyo tunaishi huku ni upendo mkubwa na kila mchezaji anafurahi maisha yake hapa.


“Malipo yao ni uhakika na uwezo wao ni mkubwa ndani ya uwanja. Nina amini kwamba kwa msimu huu tutafanya makubwa na mashabiki watapenda hivyo waendelee kutupa sapoti,” amesema.


Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 baada ya kucheza mechi 9 za ligi kibindoni ina pointi zake 11.


Imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba leo Novemba 5 inasaka pointi tatu mbele ya Coastal Union.

SOMA NA HII  YANGA KIGELEGELE AWAOMBA MASHABIKI KUACHA MIHEMUKO