Home Uncategorized YANGA YAIPIGA KIJEMBE KIMTINDO SIMBA ISHU YA CHAMA

YANGA YAIPIGA KIJEMBE KIMTINDO SIMBA ISHU YA CHAMA

 


MENEJA wa kikosi cha Yanga, Hafidhi Saleh, amesema kuwa Yanga haihusiki kwa namna yoyote na makosa ya mwamuzi wa mchezo wa dabi, Abdallah Mwinyimkuu huku akiamini makosa hayo yalifanyika kutokana na upungufu wa kibinadamu.

 

Baada ya mchezo huo ulioisha kwa sare ya bao 1-1, viongozi na mashabiki mbalimbali wa Simba wamekuwa wakitupa tuhuma kali kwa Mwinyimkuu kwa kushindwa kutafsiri kwa ufasaha Sheria 17 za mchezo huo, huku akiishia kuamuru penalti iliyowapa faida Yanga, licha ya tukio hilo kuonekana kuwa na utata.

 

Saleh amesema: โ€œSimba mara zote wamezoea kulalamika, nadhani kuna daraja wamejiweka wanaamini wao sio timu ya kufungwa au hata kutoa sare na ndiyo maana utawaona sio tu kwenye mchezo wa Jumamosi, Simba walilalamika walipofungwa dhidi ya Tanzania Prisons na hata Ruvu Shooting.

 

โ€œKwangu mimi sioni kama kulikuwa na tatizo lolote kwa mwamuzi zaidi ya ukweli kuwa kuna wakati mwamuzi kama binadamu anaweza kufanya makosa ya kibinadamu na ndicho ambacho kilitokea, hivyo sidhani kama kulikuwa na ulazima wa kumlalamikia mwamuzi au wachezaji.

 


โ€œKwa kweli nimeshangazwa kuona kiongozi mmoja mkubwa tu wa kikosi hicho akiwashutumu baadhi ya wachezaji wao akiwemo Chama, (Clatous) kuwa walicheza chini ya kiwango eti kwa kuwa wanahusishwa kujiunga na Yanga, hili sio jambo sahihi.โ€


Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 24, Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20 zote zimecheza mechi 10.


Chanzo: Championi

SOMA NA HII  MUONEKANO WA GAZETI LA SPOTI XTRA KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMAPILI