Home Uncategorized ZILIZOSHUKA LIGI KUU BARA ZINA MAISHA MAGUMU FDL

ZILIZOSHUKA LIGI KUU BARA ZINA MAISHA MAGUMU FDL

 


TIMU nne ambazo zilikuwa zinashiriki Ligi Kuu Bara maisha yao ndani ya Ligi Daraja la Kwanza, (FDL) ni magumu kwa kuwa bado hazijaonyesha matumaini ya kurejea kwenye mstari kwa msimu ujao kutokana na mwendo wa kusuasua walioanza nao.

Ukiiweka kando Lipuli iliyoshuka baada ya kufikisha pointi 44 anza na Singida United iliyoshuka ikiwa na pointi 18, Mbao FC iliyoshuka na pointi 45 sawa na Alliance huku Ndanda wao walishuka na pointi 41 hawa wameanza kwa kubwana mbavu.

Singida United imecheza mechi nne ipo nafasi ya nane ina pointi mbili kibindoni , imepata sare mbili na kuchapwa mechi mbili. Mbao ipo nafasi ya tisa na Alliance ipo nafasi ya 10 hizi mbili hazijui ladha ya sare wala ushindi.

Safu zote za ushambuliaji za timu ya Singida United, Mbao FC na Alliance zimetupia bao mojamoja ndani ya kundi B ambalo kinara ni Geita Gold mwenye pointi 12.

Mbao imefungwa mabao saba, Singida United imefungwa mabao manne na Alliance imefungwa mabao 10 ndani ya dakika 360 walizoshuka uwanjani.

Kwa upande wa kundi A Ndanda FC wao wapo nafasi ya 10 wakiwa na pointi mbili baada ya kuambulia sare mbili huku wakiambulia kichapo mechi mbili na safu yao ya ushambuliaji imefunga mabao mawili, kundi A kinara ni African Sports ana pointi 12 anafuatiwa na Lipuli ambaye yupo nafasi ya pili na pointi 10 kibindoni.

 

SOMA NA HII  AZAM VS YANGA NI MECHI YA KISASI