Home Uncategorized BENCHI KUMUONDOA KIPA SIMBA

BENCHI KUMUONDOA KIPA SIMBA


KIPA namba tatu wa Klabu ya Simba, Salim Juma anatajwa kuwa kwenye hesabu za kutolewa kwa mkopo ndani ya timu hiyo Kwenye dirisha dogo ambalo limefunguliwa Desemba 16.


Juma amekuwa akikosa nafasi kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba jambo linalomfanya azidi kujenga ushkaji na nyavu.


Ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2020/21 hajakaa langoni kwenye mechi hata moja ya Simba. 


Miongoni mwa timu zinazopewa chapuo ya kumhitaji nyota huyu kwa mkopo ni pamoja na Coastal Union ya Juma Mgunda na Mwadui FC.

SOMA NA HII  BREAKING: SARRI AFUNGASHIWA VIRAGO JUVENTUS