Home Uncategorized CRISTIANO RONALDO ATUMA SALAMU ZA CHRISTMAS

CRISTIANO RONALDO ATUMA SALAMU ZA CHRISTMAS


NYOTA wa Klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo ametuma ujumbe wa salamu za Christmas kwa mashabiki wake duniani licha ya kwamba timu yake inapambana ili kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu ya nchini Italia maarufu kama Seria A.

Kwa sasa Juventus haitacheza mchezo wowote kutokana na mapumziko ya ligi kwenye kipindi hiki cha baridi na itacheza na Klabu ya Udinese iliyo nafasi ya 12 na pointi 15 huku yenyewe ikiwa nafasi ya 6 na pointi 24 kinara akiwa ni A.C Milan mwenye pointi 34 

Ikiwa leo ni sikukuu ya Christmas duniani ambayo ni kumbukizi ya kuzaliwa Yesu Kristo, Ronaldo ametuma picha yake na familia akiwa na rafikiye Georgina Rodriguez pamoja na watoto wake wanne wakiwa kwenye mti wa Christmas.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 35 amesema kuwa anawatakia kila kheri ya Christmas, afya njema na furaha tele siku ya leo ambayo imejaa upendo.

Mbali na Ronaldo pia staa wa Klabu ya Atletico Madrid, Luis Suarez naye pia alituma picha akiwa na familia yake pamoja na staa wa Klabu ya Manchester City Kevin De Bruyne naye alifanya hivyo ikiwa ni furaha ya kuwatakia mashabiki zake kheri kwenye sikukuu ya leo.


SOMA NA HII  KMC KIMATAIFA USO KWA USO NA NYOTA WA SIMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here