Home Uncategorized KAGERE AKANUSHA KUGOMBANA NA BOCCO

KAGERE AKANUSHA KUGOMBANA NA BOCCO

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Simba, Meddie Kagere ameungana na nahodha wake John Raphael Bocco kukanusha uvumi wa kuwepo ugomvi kati yao.

Kagere na Bocco walikuwa sehemu ya kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania jana Jumatano, huku tukio la kupishana kwa Bocco na Kagere wakati wa kushangilia bao la Chama likiibua Sintofahamu ya kutokuelewana kwa wawili hao.

Kagere kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram amesema: “Ningependa kuwa mkweli juu ya Suala hili linaonihusisha mimi na nahodha wangu John Bocco, kwa heshima kubwa niseme sijawahi kuwa na tatizo lolote na Bocco wala mchezaji yeyote wa Simba.

“Kwa upande wangu ni bora tukapambana na wapinzani wetu kuliko kupambana sisi wenyewe. Ni matumaini yangu kuwa mmenielewa na nawashukuru sana,”

SOMA NA HII  SIMBA vs WYDAD NI KISASI NA HESHIMA MASTAA WATOA TAMKO