Home Uncategorized KIUNGO FUNDI WA SIMBA ANUKIA IHEFU FC

KIUNGO FUNDI WA SIMBA ANUKIA IHEFU FC


 UONGOZI wa Klabu ya Ihefu FC umetuma maombi kwa Klabu ya Simba ili kupata huduma ya kiungo mshambuliaji Miraji Athuman kwa mkopo.

Habari zimeeleza kwamba Ihefu inayopambana kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22 imetazama namna mambo yanavyokwenda na kuona kwamba ni lazima ipate kiungo mwenye uwezo wa kutengeneza mipango na kufunga.

Mchezo wake uliopita mbele ya Yanga wa kufungia raundi ya kwanza ilinyooshwa mabao 3-0 huku safu yake ya ushambuliaji na kiungo ikishindwa kutengeneza mipango makini.

Mtoa taarifa ameeleza kuwa miongoni mwa nyota ambaye anatakiwa ndani ya Ihefu ni Miraji Athuman.

“Mabosi wa Ihefu wamegundua kwamba mwendo wao sio mzuri hivyo wametuma maombi Simba wapewe Miraji kwa mkopo.

“Kutokana na nafasi yake ndani ya Simba kuwa finyu huenda akaibukia ndani ya Ihefu ambako huko atakuwa na uhakika wa namba kikosi cha kwanza,” ilieleza taarifa hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ameweka wazi kwamba kuna nyota ambao watatolewa kwa mkopo ili wapate nafasi za kucheza.


Ihefu ipo nafasi ya 17 ikiwa imecheza mechi 17 ina pointi 13.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR: AZAM FC WALIKUWA WANAKUTANA NA TIMU NDOGO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here