Home Uncategorized KOCHA SIMBA AINGIA ANGA ZA YANGA

KOCHA SIMBA AINGIA ANGA ZA YANGA


SELEMAN Matola, Kocha Msaidi wa Klabu ya Simba anatajwa kuingia anga za Azam FC ambao wanasaka mbadala wa Aristica Cioaba


Cioaba alifutwa kazi Novemba 26 ikiwa ni siku moja baada ya timu ya Azam FC kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga, mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex. 


Kwa sasa Azam FC ipo chini ya Kocha Msaidizi, Vivier Bahati na mchezo wake wa Kwanza alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume.


Cioaba kabla ya kufutwa kazi alipoteza mechi mbili mfululizo alianza kufungwa bao 1-0 dhidi ya KMC kisha akapoteza mbele ya Yanga jambo lililowafanya mabosi wake kumfungia virago.


Habari zinaeleza kuwa kabla ya kuongeza mkataba ndani ya Azam FC, Matola alikuwa kwenye mazungumzo na Azam FC ila dili lake lilibuma kutokana na mwendo ambao alianza nao raia huyo wa Romania.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kwa sasa majina mengi yanatajwa hivyo mashabiki wasiwe na mashaka kila kitu kitakuwa sasa.


“Kuna majina mengi kweli kwa sasa yanatajwa ila hakuna tatizo kwa sababu Azam FC ni timu kubwa, mchakato unaendelea na baada ya muda kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.

SOMA NA HII  BALAA LA NAMUNGO NA YANGA LEO ACHA KABISA MAJALIWA