Home Uncategorized KUMBE WACHEZAJI AZAM FC HAWAELEWI

KUMBE WACHEZAJI AZAM FC HAWAELEWI

 


VIVIER Bahati, kocha msaidizi wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wamekuwa hawaelewi nini cha kufanya pale wanaposhinda mapema kwa kuanza kujilinda ilihali wana kazi ya kutafuta ushindi.

Mara ya mwisho Azam FC kushinda ilikuwa ni Novemba 5 ilishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Azam Complex baada ya hapo ikiwa imecheza mechi sita mfululizo, imepoteza mechi mbili na kulazimisha sare nne.

Mechi zake ilikuwa namna hii:-KMC 1-0 Azam FC, Uwanja wa Uhuru. Azam 0-1 Yanga,Uwanja wa Azam Complex.Biashara 1-1 Azam FC, Uwanja wa Karume.

Gwambina 0-0 Azam FC,Uwanja wa Gwambina Complex. Azam FC 2-2 Namungo FC, Azam Complex.
Azam 2-2 Ruvu Shooting, Azam Complex.

Mechi mbili mfululizo ilizopata sare Uwanja wa Azam Complex ilianza kushinda na matokeo yake yalipinduliwa jambo lililoifanya timu hiyo kubaki nafasi ya tatu na pointi 29 baada ya kucheza mechi 16.

Vivier amesema:”Wachezaji wamekuwa hawaelewi nini cha kufanya pale ambapo wanapata ushindi mapema. Jambo hilo linawafanya wawe wanapiga pasi nyingi  fupi za nyuma wakati tumewaambia kwamba wanapaswa wapeleke mipira mbele kushambulia,” .

SOMA NA HII  MBELGIJI AWAPIGA MKWARA NYOTA HAWA WA YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here