Home Uncategorized MBELGIJI SIMBA AKWAA KIZINGITI CHA KUFUNGIA MWAKA

MBELGIJI SIMBA AKWAA KIZINGITI CHA KUFUNGIA MWAKA


 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba leo wanakutana na ngoma nzito ya kufungia mwaka 2020 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa ambao ni Ihefu FC.

Ikiwa kwenye presha ya kupunguza pointi inazodaiwa na watani zao wa jadi Yanga inakutana na Ihefu ambayo inapambania nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa ipo nafasi ya 16 na pointi zake 13 baada ya kucheza mechi 17.

Simba ipo nafasi ya pili na pointi 32 baada ya kucheza mechi 14 imeachwa kwa jumla ya pointi 11 na watani zao wa jadi Yanga ambao wana pointi 43 baada ya kucheza mechi 17.

Sven anakutana na ngoma nzito kwa kuwa anakutana na benchi la ufundi la Ihefu linaloongozwa na Zuber Katwila ambaye alimbania pointi tatu Uwanja wa Jamhuri wakati ule akiifundisha Mtibwa Sugar kwenye sare ya kufungana bao 1-1.

Kizingiti kingine anachokutana nacho ni kipa namba moja wa Ihefu ambaye ni Deogratius Munish, ‘Dida’ amekaa ndani ya Simba kwa muda wa msimu mmoja, 2018/19 hivyo anajua mbinu za wapinzani wake jambo litakaloongeza ugumu.

Sven Vandenbroeck ambaye amewaka kuhusu ubora wa wachezaji wake akitaka kubebeshwa lawama zote yeye mwenyewe ameliambia amesema kuwa kila mchezo kwake anahitaji pointi tatu.

“Tunahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo ambao tunaingia uwanjani na lengo ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya ili kuzidi kufuata malengo ambayo tumejiwekea,” .

Katwila Kocha Mkuu wa Ihefu amesema kuwa maandalizi yapo vizuri ni suala la kusubiri wakati ili wapate kile wanachokistahili.

SOMA NA HII  NYOTA KAGERA SUGAR APANIA MAKUBWA VPL