Home Uncategorized ORODHA YA WACHEZAJI WATANO WA SIMBA WALIOITWA STARS

ORODHA YA WACHEZAJI WATANO WA SIMBA WALIOITWA STARS

 


NYOTA watano wa kikosi cha kwanza cha Simba wameitwa ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kinachonolewa na Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije.


Nyota hao ni kipa namba moja Aish Manula, beki wa kulia Shomari Kapombe beki kiraka Erasto Nyoni naye jina lake limejumuishwa kikosini.


Wengine wawili ni kiungo Said Ndemla mwenye sifa ya kupiga mashuti yenye uzito akiwa nje ya 18 na mshambuliaji bora wa muda wote ndani ya Bongo, John Bocco mwenye zaidi ya mabao 100. 

Kikosi cha Stars kinatarajiwa kuingia kambini Januari Mosi kwa ajili ya maandalizi ya Chan 2021 ambapo kitacheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa na timu ya Congo.

SOMA NA HII  AZAM FC YAENDELEZA UBABE UGENINI, YAJIPIGIA 1-0 TANZANIA PRISONS