Home Uncategorized RASMI,MANULA NA BOCCO KUIKOSA FC PLATINUM

RASMI,MANULA NA BOCCO KUIKOSA FC PLATINUM


SVEN Vandenbroeck amesemakuwa nyota wawili ambao ni John Bocco nahodha wa timu na kipa namba moja Aishi Manula watakosekana kwenye mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe. 


Sven amesema:-“Tunamasaa machache kabla ya mchezo, tumejaribu kila kitu ili wawe tayari kwa mchezo lakini itakuwa ngumu kuwa tayari. 

“John [Bocco] bado yupo kitandani hayupo sawa, Aishi aliumia mchezo uliopita na anaweza kuchukua wiki au zaidi ili kuwa sawa. Mpaka sasa kuna uwezekano asilimia 50 ya kuwepo kwenye mchezo.”


Ikiwa Manula hatakuwa fiti mpaka kesho mikoba yake  anaweza kuchukua Ally Salim ama Beno Kakolanya. 

SOMA NA HII  GAMONDI ATUMIA DIRISHA DOGO KUWANYOOSHA MASTAA YANGA