Home Uncategorized REKODI YA SIMBA KUTIBULIWA NA MWADUI YAMPA SOMO KAZE

REKODI YA SIMBA KUTIBULIWA NA MWADUI YAMPA SOMO KAZE

 


CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ataingia uwanjani leo Desemba 12 kwa tahadhari kubwa wakati wakusaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC kwa kuwa anatambua ni watibua rekodi wazuri.


Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 14 haijapoteza mchezo inakutana na Mwadui FC ambayo imeshinda mechi tatu na kupoteza mechi 10 ikipata sare moja.


Kaze ameweka wazi kwamba licha ya kasi aliyonayo anawakumbuka Mwadui walitibua rekodi ya Simba kutofungwa msimu wa 2019/20.


“Mwadui ni timu nzuri licha ya kwamba haipati matokeo chanya, niliifuatilia msimu uliopita ilitibua rekodi ya Simba kutofungwa hivyo nimewaambia vijana wawe makini.


“Tunahitaji ushindi ili tuzidi kuwa imara ila hatupaswi kuwadharau wapinzani wetu kwa namna yoyote ile lazima tunawaheshimu,” .


Yanga ipo nafasi ya kwanza ina pointi 34 inakutana na Mwadui FC yenye pointi 10 nafasi ya 17.


Mchezo wa leo utachezwa Uwanja wa Kambarage,  Shinyanga.

SOMA NA HII  COASTAL UNION YAMKOMALIA KIBA