Home Uncategorized SIMBA KUIFUATA MBEYA CITY LEO

SIMBA KUIFUATA MBEYA CITY LEO

KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Sven Vandenbroeck leo Desemba 11 kimeanza safari kuelekea Mbeya.


Kitashuka Uwanja wa Sokoine Desemba 13 kumenyana na Mbeya City ambayo inakwenda mwendo wa kusuasua, Uwanja wa Sokoine. 

Mbeya City ikiwa imecheza jumla ya mechi 14 ndani ya ligi imeshinda mbili na kupoteza sita sawa na ile iliyopata sare ikiwa nafasi ya 15 na pointi 12.

Msimu uliopita mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Simba ilishinda mabao 2-0.


Mabao yote yalifungwa na nahodha John Bocco ambaye ni mchezaji bora kwa mwezi Novemba na kuifanya timu hiyo kusepa na pointi tatu.


Hivyo mchezo ujao, Mbeya City itaingia ndani ya uwanja ikiwa na hasira za kulipa kisasi cha kupoteza kwenye mechi zote mbili zilizopita msimu uliopita kwa sababu ule wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0 Uwanja wa Uhuru.


Simba itaingia ndani ya uwanja ikiwa na presha ya kupambania taji ambalo linaonekana kuwa zito kwa sasa kwa kuwa wapinzani wake Yanga wapo nafasi ya kwanza na pointi 34.

Ikiwa ipo nafasi ya tatu na pointi 26 ina mzigo mzito wa kumaliza viporo viwili ili iwe sawa na Yanga huku ikitakiwa kushinda zote na hata ikishinda bao itakuwa na deni la pointi.


Kama itatokea Simba ikashinda mechi zake mbili za viporo itafikisha pointi 32 na kubakiwa na deni la pointi mbili kuifikia Yanga jambo ambalo linazidi kuongeza uzito kwenye mchezo huo.


Yanga ikiwa imecheza mechi 14 haijapoteza mchezo tofauti na Simba ambayo imepoteza mechi mbili mfululizo na kufanya ipoteze jumla ya pointi sita zinazoiweka timu hiyo kwenye presha ya kusaka ushindi kila mchezo.

Vandenbroeck amesema kuwa wanahitaji ushindi ili kupata pointi tatu kwenye mechi zao zote ili kuwafikia wapinzani wao.


Ofisa Habari wa Mbeya City, Shaha Mjanja amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani.

SOMA NA HII  ZAHERA WA YANGA KUSHUSHA JEMBE MOJA LA KAZI