Home Uncategorized SIMBA V POLISI TANZANIA TAMBO TUPU KWA WABABE HAWA

SIMBA V POLISI TANZANIA TAMBO TUPU KWA WABABE HAWA



KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo Uwanja wa Mkapa dhidi ya Polisi Tanzania.

Ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo, Simba inakutana na Polisi Tanzania ambayo ipo nafasi ya sita.


Mabingwa watetezi ambao ni Simba kibindoni wana pointi 23 baada ya kucheza mechi 11 huku Polisi Tanzania ikiwa na pointi 20 baada ya kucheza mechi 13.


Raia huyo wa Ubelgiji anakutana na mzawa Malale Hamsini ambaye kasi yake ya kusaka matokeo ndani ya uwanja ipo vizuri.


Mtambo wa mabao kwa Simba ni John Bocco akiwa na mabao saba huku wa Polisi Tanzania ni Marcel Kaheza mwenye mabao matatu.


Sven amesema:”Wachezaji wapo vizuri na wanatambua kwamba tuna kazi ya kupunguza idadi ya pointi ambazo tunadaiwa, tutaingia ndani ya uwanja kusaka pointi tatu kwa juhudi,”.


Hamsini amesema:”Ni suala la muda, tunajua aina ya timu ambayo tunakwenda kukutana nayo ni imara nasi pia tupo imara,”.

Msimu uliopita mchezo wa mwisho walipokutana uwanjani, Simba ilishinda mabao 2-1 Uwanja wa Ushirika, Moshi.

SOMA NA HII  AZAM NAO KUKIWASHA USIKU DHIDI YA SIMBA, TAIFA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here