Home Uncategorized SIMBA WAITWA MEZANI KUPEWA MBADALA WA MUGALU

SIMBA WAITWA MEZANI KUPEWA MBADALA WA MUGALU

UONGOZI wa Gwambina FC umewaita mabosi wa Simba mezani ili kujadili juu ya suala la kumpata mshambuliaji wao namba moja, Meschak Abraham ili abebe mikoba ya Chris Mugalu ambaye anasumbuliwa na majera.

Hivi karibuni imeelezwa kuwa Simba inayonolewa  na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ipo kwenye hesabu za kuipata saini ya Abraham Meshack ambaye anavutana shati na Jonh Bocco kwenye chati ya ufungaji.

Meshack ndani ya Gwambina ambayo ipo nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 12 na kufunga mabao 12 amefunga mabao sita huku Bocco akiwa amefunga mabao saba.




Akizungumza na Spoti Xtra, Mratibu wa Mashindano ndani ya Gwambina FC, Mohamed Almas alisema kuwa bado hawajapata ofa kuhusu mchezaji wao zaidi ya kuskia tetesi tu.

“Mpaka sasa hakuna timu iliyokuja na ofa kwa ajili ya kumpata nyota wetu Meschak hata hao Simba tunaskia tu, ila ikiwa watakuja basi tutakaa mezani kuzungumza ili tuone itakujae kwani hata sisi pia tuna malengo yetu,” alisema.


Kwa sasa Simba imeshaanza mchakato wa kufanya usajili kwenye dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15.


Imeshamtambulisha nyota mmoja ambaye ni kiungo mkabaji raia wa Uganda ambaye anarithi mikoba ya Gerson Fraga Taddeo Lwanga.

SOMA NA HII  MTOTO ALIYEPOTEA SIKU SITA DAR APATIKANA ARUSHA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here