Home Uncategorized SIMBA YAMKINGIA KIFUA SVEN VANDENBROECK

SIMBA YAMKINGIA KIFUA SVEN VANDENBROECK


 CLATOUS Chama, ametetea mbinu zilizotumiwa na kocha wao, Sven Vandenbroeck katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United uliopigwa Jumamosi iliyopita kwa kusema mbinu hizo ndizo zimesababisha wafuzu hatua ya kwanza ya michuano hiyo.

 

Simba imefuzu kwa matokeo ya jumla ya ushindi wa bao 1-0 na sasa inatarajiwa kucheza dhidi ya Platinum FC ya Zimbambwe, ambayo nayo imefuzu hatua hiyo kwa kuwaondosha Costa do Sol ya Msumbiji.

 

Licha ya Simba kufuzu mijadala imekuwa mingi kutokana na mbinu zilizotumiwa na Simba ambao walionekana kuzuia zaidi kuliko kutengeneza nafasi za kufunga.

 

Mzambia huyo amesema kuwa iliwapasa kucheza kwa tahadhari kubwa na kuhakikisha wanalinda mtaji wa bao 1-0 walilolipata nchini Nigeria kwa kuwa lilikuwa limebeba tiketi ya kufuzu hatua inayofuata.

 

“Tuliingia katika mchezo wa Jumamosi tukiwa tayari tuna faida ya bao 1-0 tulilolipata ugenini kule Nigeria, hivyo tulijua wazi kuwa kama tunaweza kujitahidi na kuhakikisha haturuhusu bao hapa nyumbani basi tungefuzu na kuwaondosha Plateau.

 

“ Sven alituelekeza pia na imetusaidia kuingia hatua ya kwanza ya michuano hii, unajua katika hatua hizi za mtoano mbinu kubwa ni kuhakikisha unapata matokeo na kufuzu kuelekea hatua inayofuata.

 

“Kwani unaweza kucheza mpira mzuri lakini kama utakosa matokeo na kuondolewa kwenye mashindano, kucheza vizuri kwako hakuwezi kuwa na faida, hivyo kwangu mimi nawapongeza wachezaji wenzangu na Wanasimba kiujumla kwa kuwa tumerekebisha makosa ya msimu uliopita na tunasonga mbele,” amesema Chama.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YAZITAKA SIMBA NA YANGA ZIJIPANGE KUINGIA ANGA ZAO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here