Home Uncategorized SOLSKJAER AWASIFU WACHEZAJI WAKE

SOLSKJAER AWASIFU WACHEZAJI WAKE

 


KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa vijana wake walipambana mwanzo mwisho kusaka pointi tatu mbele ya Leeds United jambo ambalo walifanikiwa kwa asilimia 100.

Ikiwa Uwanja wa Old Trafford usiku wa kuamkia leo Desemba 21, Manchester United ilishinda kwa mabao 6-2 dhidi ya Leeds United ndani ya Ligi Kuu England. 

Scott Mc Tominay dakika ya 2 na 3, Bruno Fernandes dakika ya 20 na dakika ya 70 kwa mkwaju wa penalti hawa walipachika mabao mawilimawili huku Victor Lindelof dakika ya 37 na Daniel James dakika ya 66 walipachika bao mojamoja.


Kwa upande wa Leeds United mabao yao yalipachikwa na Liam Cooper dakika ya 41 na Stuart Dallas dakika ya 73 na kuifanya ibaki na pointi 17 ikiwa nafasi ya 14 na United inakuwa ndani ya tatu bora ina pointi 26.

Solskjaer amesema:”Tumeweza kubakiza pointi tatu muhimu nyumbani hili ni jambo jema na tunapaswa kuwa na muendelezo bora, wachezaji wangu walicheza vizuri wanahitaji pongezi”.

SOMA NA HII  BABA MANARA AFUNGUKA USAJILI WA YANGA, MASHABIKI WA YANGA NI WENGI