Home Uncategorized WAMISRI WAMKOMALIA KICHUYA KONA WA SIMBA, FIFA KUSHUSHA RUNGU KWA SIMBA

WAMISRI WAMKOMALIA KICHUYA KONA WA SIMBA, FIFA KUSHUSHA RUNGU KWA SIMBA


 IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Namungo FC inayoshiriki Kombe la Afrika ikiwa imepenya hatua ya mchujo, Shiza Kichuya amefungiwa kuendelea kutumika ndani ya kikosi hicho.


Habari zinaeleza kuwa nyota huyo wa zamani wa Simba alisajiliwa na timu hiyo akiwa na mkataba na Klabu ya Pharco ya Misri.


Kichuya alipata umaarufu ndani ya Simba kutokana na kufunga bao la kona lililozama mazima kwenye nyavu wakati timu hiyo ilipocheza na Yanga, ambao ni watani zao wa jadi.

Alijiunga na Klabu hiyo msimu wa 2018 akitokea ndani ya Simba na alisepa kimyakimya kutokana na kukosa namba ya kudumu kikosi cha kwanza ambapo alicheza jumla ya mechi 3 pekee.


Alirejea Simba msimu wa 2019/20 ambapo alisaini dili la miezi sita hivyo kwa kosa hilo inaelezwa kuwa Simba imepigwa faini na FIFA.

Habari kutoka chanzo cha ndani ya Namungo imesema kuwa taarifa hizo zipo mezani hivyo wanazifuatilia ili kujua hatma yao itakuaje juu ya mchezaji huyo pamoja na suala la mkataba wake wa awali.


Tayari ndani ya Namungo Kichuya ameanza kujenga ushkaji na nyavu ambapo kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Rabita ya Sudan Kusini uliochezwa Uwanja wa Azam Complex alitupia bao moja wakati timu yake ya Namungo ikishinda mabao 3-0.

Pia Uwanja wa Mkapa wakati timu yake ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Yanga alisababisha penalti moja iliyookolewa na kipa namba moja wa Yanga, Metacha Mnata.

SOMA NA HII  SIMBA KUFANYA MABADILIKO HAYA MAWILI