Home Uncategorized YANGA YAMVUTIA KASI BEKI WA AS VITA

YANGA YAMVUTIA KASI BEKI WA AS VITA

 


OUSMANE Adama Ouattara beki kitasa wa Klabu ya AS Vita ya Congo anatajwa kuingia kwenye rada za mabosi wa Yanga.


Licha ya Yanga kutokuwa na shida kwenye nafasi ya ulinzi kwa sasa habari zinaeleza kuwa mpango mkubwa wa kikosi hicho ni kuwa na wachezaji matata hata wale watakaokaa benchi.


Ikiwa inaongoza Ligi Kuu Bara na pointi 43 imefungwa mabao sita kati ya mechi 17 kwa msimu wa 2020/21 na safu yao ya ulinzi inaongozwa na nahodha Lamine Mono raia wa Ghana.


Moro amekuwa akishirikiana na Bakari Mwamnyeto ambaye ni mzawa kuweka lango salama la Yanga inayohitaji ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.


Nyota huyo ni raia wa Ivory Coast ana umri wa miaka 27 hivyo huenda dili likitimia wataunda ukuta matata ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Cedric Kaze.


Kocha Kaze kuhusu usajili amesema kuwa anahitaji kuongeza wachezaji wachache ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake.


“Sitahitaji kuwa na wengi kwenye dirisha dogo ila wachezaji wachache ambao wataingia moja kwa moja kikosi cha kwanza,” .

SOMA NA HII  MASHINE NYINGINE YA KAZI HII HAPA KUTUA SIMBA