Home Uncategorized ARSENAL YATEMBEZA 4G, LACAZETTE NI NAMBA MOJA

ARSENAL YATEMBEZA 4G, LACAZETTE NI NAMBA MOJA


 ALEXANDRE Lacazette nyota wa Arsenal ni namba moja kwa utupiaji ndani ya kikosi hicho baada ya kufikisha jumla ya mabao 7 katika mechi 14 za Ligi Kuu England ambazo amecheza. 


Wakati Arsenal ikishinda kwa mabao 4-0 ugenini dhidi ya West Brom alitupia mabao mawili dakika ya 60 na 64 na yake mengine mawili yalitupiwa na Kieran Tierney dakika ya 23 na Bukayo Saka dakika ya 28.


Lacazette anachojua yeye ndani ya uwanja  ni kucheka na nyavu tu kwani katika mabao yote hayo saba aliyotupia hajatengeneza pasi ya bao.


Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kufikisha jumla ya pointi 23 ikiwa nafasi ya 11 huku West Brom ikiwa nafasi ya 19 na pointi zake 8.


Mikel Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa bado wana kazi ya kufanya kufikia mafanikio ambayo wanahitaji.

SOMA NA HII  JESHI LA KAGERA SUGAR DHIDI YA SIMBA