Home kimataifa ARTETA AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUONGEZA KUJIAMINI

ARTETA AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUONGEZA KUJIAMINI

 MIKEL Arteta,  Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa wachezaji wake wana kazi ya kulinda viwango vyao ili kuendelea kupata ushindi kwenye mechi zao zote zijazo pamoja na kuongeza hali ya kujiamini.

Arsenal ikiwa Uwanja wa Emirates iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Newcastle United jambo ambalo limemfurahisha Arteta. 

Mabao ya Arsenal yalifungwa na nahodha Pierre Emerick Aubameyang ambaye alifunga mawili dakika ya 50 na 77 na bao moja alifunga Bukayo Saka dakika ya 60.

Ushindi huo unaifanya Arsenal kufikisha jumla ya pointi 27 ikiwa nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 19 huku Newcastle ikiwa nafasi ya 15 na pointi 19 baada ya kucheza mechi 18. Kinara ni Manchester United inayonolewa na Ole Gunner Solskjaer ikiwa na pointi 37 ambaye amesema kuwa wachezaji wake walipambana mithili ya kupanda mlima Kilimanjaro.

Arteta amesema:”Muhimu kwa wachezaji kupambana na kupata ushindi jambo hilo litawaongezea hali ya kujiamini hivyo wanatakiwa kushika hapo ambapo wapo,”.

SOMA NA HII  MBAPPE AFICHUA ALIVYOITOSA LIVERPOOL....PAMOJA NA MAMA YAKE KUINGILIA KATI LAKINI WALITOKA 'KAPA'....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here