Home Uncategorized BEKI STARS AKUBALI KUSAINI DILI JIPYA NDANI YA YANGA

BEKI STARS AKUBALI KUSAINI DILI JIPYA NDANI YA YANGA


 BEKI wa Klabu ya Mtibwa Sugar, Dickson Job ambaye kwa sasa yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayojiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Congo unaotarajiwa kuchezwa kesho, Uwanja wa Mkapa amesema kuwa hana tatizo ikiwa Yanga watahitaji saini yake.


Imekuwa ikielezwa kuwa Yanga inayonolewa na Cedric Kaze inahitaji huduma ya nyota huyo ambaye ni beki wa kati ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi.

Beki huyo pia msimu uliopita alitajwa kuwekwa kwenye rada za Yanga ila mambo yalikwenda tofauti na mwisho wa siku Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union alisaini dili la kuitumikia timu hiyo.

Job amesema:”Naskia kwamba Yanga wanahitaji saini yangu ila bado haijawa rasmi kwa sasa kuja mezani kuzungumza.

“Ikiwa ni kweli mimi sina tatizo nitasaini ndani ya Yanga ila muhimu ni kuweza kufuata utaratibu kwa kuweza kuzungumza na uongozi wa timu yangu,” .

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kuhusu usajili suala hilo linategemea ripoti ya kocha.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR; TIMU ZOTE ZIUNGANE KUPAMBANA NA CORONA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here