Home Yanga SC KOCHA YANGA AIKANA SIMBA

KOCHA YANGA AIKANA SIMBA


KOCHA msaidizi wa klabu ya Yanga, Nizar Khalfani amekanusha taarifa za baadhi ya watu wanaosema kuwa ana mapenzi na Simba  kwa kusema kuwa hana mapenzi yoyote na Simba kwani yeye ni shabiki wa Yanga.

Taarifa hizo zilikuwa zikipewa nguvu na kipande cha video ambayo ilikuwa ikimuonyesha Nizar akisifia uwezo wa nyota wa Simba kucheza soka la kuvutia kwenye moja ya mahojiano aliyowahi kuyafanya miaka kadhaa iliyopita.

Nizar pamoja na kocha mpya wa viungo Edem Mortotis walitambulishwa rasmi na Yanga jana Jumatano kuchukua nafasi za aliyekuwa kocha msaidizi, Juma Mwambusi na Riedoh Berdien aliyewahi kuhudumu kama kocha wa viungo na utimamu wa mwili.

Nizar na Mortotsi wamejiunga na Yanga kuimarisha benchi la ufundi kwa ajili ya kuwa na kikosi imara ambacho kitafanikisha lengo lao la kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kombe la FA. 

Akitolea ufafanuzi taarifa hizo Nizar amesema: “Nimekuja kuisaidia Yanga katika malengo yake ya kutwaa ubingwa msimu huu, najua kuna kipande cha video inayosambazwa mitandaoni ikinionyesha nikisifia Simba laikini napenda kuweka wazi kuwa sina mapenzi yoyote na klabu ya Simba,” 

SOMA NA HII  WAKATI SAKHO AKIZIDI KUKIWASHA SIMBA...NKANE APATA 'PANCHA' YANGA...UONGOZI WAJA NA HOJA HIZI...