Home Simba SC MATOLA : MORRISON HAKUWA FITI.!!

MATOLA : MORRISON HAKUWA FITI.!!

 


Wakati mashabiki wengi wa Simba wakionekana kutaka kumwona winga wao Bernard Morrison akicheza kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi kocha Seleman Matola amesema hakuwa kwenye mipango yake.

Matola alisema sababu kubwa za kutomtumia mchezaji huyo ni kutofanya mazoezi ya pamoja na wenzake kwa kipindi kirefu hivyo isingekuwa rahisi kwake kucheza kwani timu ilikuwa na malengo ya ubingwà na sio kucheza kwa kujaribu.

“Sikuona sababu ya kumtumia Morrison hata kama alikuwa kwenye wachezaji wangu wa akiba, hajafanya mazoezi kama mwezi mzima, unampangaje na analeta matokeo gani, Morrison ametoka kuumwa hivyo ni lazima awe fiti ndipo atumike.

“Sina budi kuwapongeza Yanga kutwaa ubingwa japo tumefungwa kwa penati, wachezaji wangu wamepambana kadri walivyoweza ndiyo maana dakika 90 atukufungwa,nimewatumia Hassan Dilunga na Miraji Athuman huku wakiwa wanasumbuliwa na misuli na waliniambia mapema ila sikuwa na namna,” alisema Matola ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba.

Matola alilazimika kuwatoa nafasi zao zilichukuliwa na Chris Mugalu pamoja na Ibrahim Ajibu.

SOMA NA HII  KRAMO TIA MAJI TIA MAJI MAPYA YAIBUKA SIMBA