Home Uncategorized MRUNDI KIRAKA AMALIZANA NA NAMUNGO FC

MRUNDI KIRAKA AMALIZANA NA NAMUNGO FC

 


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morroco imekamilisha dili la kupata saini ya kiungo mshambuliaji Kwizera Eric.

Nyota huyo alikuwa anakipiga ndani ya Klabu ya Olympic Star ya Burundi ni raia wa Burundi na ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya mbili ndani ya uwanja.


Namungo ambayo kwa sasa ipo Sudani kwa ajili ya mchezo wa marudio wa Kombe la Shirikisho ina mpango wa kumpata mshambuliaji atakayekuwa mbdala wa Adam Salama ambaye anasumbuliwa na majeraha.


Pia kiungo wao mpya Humud aliyejiunga na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar naye amebaki Bongo akiendelea kupata matibabu kutokana na kutokuwa fiti.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia amesema kuwa mpango wa kufanya usajili upo na ukiwa tayari utawekwa wazi kwa mashabiki.

SOMA NA HII  TOWSHIP ROLLES WAPATA MCHECHETO KWA YANGA LEO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here