Home Yanga SC SEHEMU YA CV YA KOCHA MPYA YANGA HII HAPA

SEHEMU YA CV YA KOCHA MPYA YANGA HII HAPA


KLABU ya soka ya Yanga, tayari imemtangaza, Edem Mortotis kuwa kocha wao mpya wa viungo na utimamu wa mwili ambaye anakuja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na raia wa Afrika Kusini, Riedoh Berdien aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita.

Mortotis alitua nchini siku ya Jumanne na kupokelewa na mwenyeji wake Injinia. Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa klabu ya Yanga na mjumbe wa kamati ya usajili na kwenda kusaini mkataba tayari kwa ajili ya kuanza majukumu yake mapya.

Yanga ipo kwenye mipango ya kuimarisha benchi lake la ufundi kwa ajili ya kuwa na kikosi imara ambacho kitafanikisha lengo lao la kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kombe la FA.

Hii hapa sehemu ya wasifu wa kocha huyo; 

Ni mzaliwa wa jiji la Accra Ghana, ambaye amewahi kusoma nchini Canada ambapo alikuwa akiendeleza kipaji chake cha soka na timu ya KC Trojan.

Baada ya hapo akaenda kusoma chuo cha Northern Alberta Institute of Technology cha hapo hapo Canada wakati huo anaendelea kutunza kipaji chake kupitia timu za chuo hicho.

Alipomaliza masomo yake Edem akapata nafasi ya kuitumikia timu ya akiba ya Fc Edmonton, akadumu hapo hadi 2013 alipopandishwa na kupewa mkataba na timu ya wakubwa.

Mwaka 2017 akapelekwa Edmonton Victoria akafanikiwa kucheza mechi 10 na kuifungia mabao 2, Msimu wa 2017 ulivyomalizika akajiunga na Edmonton Green & Gold akacheza mechi moja na kufunga bao moja, msimu uliofuatia wa 2018 akacheza mechi tano tu, Januari 2019 akarejea Fc Edmonton, hapo akacheza mechi 18 za Ligi baadae Novemba 2019 wakampa mkataba mpya tayari kwa msimu wa 2020

SOMA NA HII  GAMONDI AMEKUNA KICHWA KUHUSU KONKONI KISHA ASEMA HAYA