Home Uncategorized SIMBA:TUNAFUZU HATUA YA MAKUNDI AFRIKA

SIMBA:TUNAFUZU HATUA YA MAKUNDI AFRIKA


 KIPA wa Simba, Aishi Manula amefunguka kuwa kikosi chao kina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, FC Platinum ya Zimbabwe na kufuzu hatua ya makundi.

 

Simba inatarajiwa kuwakaribisha Wazimbabwe hao katika mchezo wa marudiano unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza uliopigwa Zimbabwe kwa bao 1-0.


Simba inahitaji kupata ushindi wa kuanzia mabao 2-0 ili kuweza kufuzu hatua ya makundi ambayo hawakufanikiwa kufuzu msimu uliopita baada ya kuondolewa na UD Songo ya Msumbiji katika hatua za awali.


Kipa namba moja wa Simba Manula amesema tofauti ya bao 1-0 waliyonayo mpaka sasa haiwezi kuwa kikwazo kwao kufuzu.

 

“Kwanza niseme kila mmoja anajua kuwa tuko nyuma kwa bao 1-0 mpaka sasa, lakini ni wazi bado tuna nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya makundi kwa kuhakikisha tunashinda mchezo wetu wa marudiano ambao tutacheza kwenye uwanja wa nyumbani hapa Dar es Salaam.

 

“Naamini matokeo mazuri kwenye michezo yetu miwili iliyopita yametuongezea morali ya kushinda mchezo huo, na kupitia sapoti ya mashabiki wetu na wadau wa soka hapa nchini tutafuzu na kwenda hatua ya makundi,” amesema Manula.

SOMA NA HII  MAKOCHA HAWA WAINGIA KWENYE ORODHA YA KUIBUKIA YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here