Home Taifa Stars TAIFA STARS:TUTAPAMBANA MBELE YA GUINEA LEO

TAIFA STARS:TUTAPAMBANA MBELE YA GUINEA LEO


 JOHN Bocco, nahodha wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo kwenye michuano ya Chan nchini Cameroon.

Stars ipo kundi D ina pointi tatu baada ya kucheza mechi mbili, imeshinda moja kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namibia na imepoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Zambia kwenye mchezo wa ufunguzi.

Leo itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya vinara wa kundi hilo, Guinea ambao wana pointi nne baada ya kucheza mechi mbili ili iweze kutinga hatua ya robo fainali ni lazima ipate ushindi leo saa 4:00 usiku.

Bocco amesema:”Wachezaji wamekuwa na morali kubwa mazoezini na wanajua kwamba Watanzania wanahitaji ushindi hivyo watapambana ili kufanya vizuri.

“Kikubwa tunaamini kwamba mchezo utakuwa na ushindani mkubwa hilo lipo wazi ila tutapambana ili kupata matokeo chanya Watanzania watuombee ili tufanye vizuri,” .

Bocco kuna hatihati ya kuukosa mchezo wa leo kwa kuwa yupo kwenye uangalizi maalumu wa jopo la madaktari pamoja na Ibrahim Ame ambaye ni beki.

Stars wamekuwa wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Bonamoussadi,Douala na mchezo wa mwisho wa Kundi D kwenye mashindano ya CHAN dhidi ya Guinea unatarajiwa kuchezwa leo Jumatano, Januari 27 saa 4 usiku Uwanja wa Reunification,Cameroon.

SOMA NA HII  HIKI HAPA KIKOSI CHA 'MAPRO' WA TZ WANAOWEZA KUTIKISA AFCON 2023 NA TAIFA STARS...