Home Ligi Kuu MTAMBO WA MABAO KAGERA SUGAR WAPANIA KUFANYA VIZURI

MTAMBO WA MABAO KAGERA SUGAR WAPANIA KUFANYA VIZURI


YUSUPH Mhilu, nyota anayecheza ndani ya Kagera Sugar amesema kuwa bado wana kazi ya kuendelea kupambana ndani ya uwanja ili kupata ushindi ndani ya uwanja.


Mhilu ni kinara wa utupiaji ndani ya Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Mecky Maxime.

Alikuwa miongoni mwa nyota waliofunga bao kwenye sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Yanga mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Kesho itashuka Uwanja wa Uhuru kusaka pointi tatu mbele ya KMC FC ambayo imetoka kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zote za mzunguko wa pili na watapambana kupata pointi tatu.

“Mzunguko wa pili una ushindani mkubwa na kila timu inahitaji ushindi hivyo nasi tutaingia ndani ya uwanja kusaka ushindi.

“Kikubwa mashabiki watupe sapoti ili kuona kwamba tunapata pointi tatu na kufikia malengo ambayo tumejiwekea ili kuyatimiza,” amesema.
SOMA NA HII  MKWASA ATAJA KILICHOIPOTEZA RUVU SHOOTING