Home kimataifa AUBA AMPASUA KICHWA ARTETA

AUBA AMPASUA KICHWA ARTETA


 PIERRE Emerick Aubameyang, nahodha wa kikosi cha Arsenal kwa sasa bado yupo karantini na haijulikani atarejea lini uwanjani jambo ambalo linampasua kichwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Mikel Arteta.

Raia huyo wa Gabon alitarajiwa kurejea uwanjani kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United uliokamilika kwa sare ya bila kufungana ila alikosekana ndani ya uwanja.

Auba amewekwa karantini baada ya kutoka kumjulia hali mamaye ikiwa ni kuchukua tahadhari dhidi ya janga la Corona ili kujua kwamba hajarudi na Corona.

Arteta amesema kuwa:”Alikuwa amekwenda kumuona mamaye ila kwa sasa yupo karantini hivyo tunapaswa kufuata taratibu na hatuwezi kumtumia kwa sasa,” .

SOMA NA HII  MANCHESTER UNITED MACHO YOTE KWA FATI