Home Azam FC AZAM FC:TUTARUDI KWENYE UBORA WETU

AZAM FC:TUTARUDI KWENYE UBORA WETU

 


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utapambana kusaka ushindi kwenye mechi  zao ambazo zimebaki ili kurejea kwenye ubora.

Kikosi hicho kinanolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ambaye amerithi mikoba ya Aristica Cioaba aliyechimbishwa ndani ya kikosi hicho kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mwendo mbovu wa timu hiyo.

Kilianza kwa kasi mzunguko wa kwanza ambapo kiliweza kucheza jumla ya mechi 7 mfululizo bila kupoteza na Cioaba na Dube walikuwa wa kwanza kusepa na pointi tatu mazima.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wanatambua kwamba mashabiki wanahitaji ushindi hivyo wanaamini kuwa watapata matokeo chanya kwenye mechi zao.

“Tupo imara kwani kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zetu haina maana kwamba hatupo imara tutafanya vema na tutarudi kwenye ubora.

“Kinachotokea ndani ya uwanja ni matokeo ila hakuna kibaya ndani ya uwanja, wachezaji wana morali na wanapenda kufanya kazi yao ni suala la muda.

“Imani yetu ni kwamba tutarejea kwenye ubora wetu wakati bado upo na mipango inakwenda vizuri, mashabiki watupe sapoti,”.

Mchezo uliopita Azam FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union, uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga na ingizo jipya,Mpiana Monzinzi liliaza kikosi cha kwanza baada ya kuchukua nafasi ya Obrey Chirwa ambaye ni majeruhi. 

Azam FC kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya 3 ikiwa imecheza jumla ya mechi 19 na kukusanya pointi 33.


SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGA GOLI LAKE LA KWANZA MSIMU HUU..DUBE AMCHIMBA MKWARA MAYELE...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here