Home Azam FC AZAM WAMWEKEA ULINZI DUBE

AZAM WAMWEKEA ULINZI DUBE


BENCHI la ufundi la klabu ya Azam, limeadhimia kumlinda mshambuliaji wao hatari raia wa Zimbabwe, Prince Dube kwa kumpunguzia baadhi ya majukumu yanayoweza kumsababishia arudi kwenye majeruhi.

Dube alirejea uwanjani Januari 17, mwaka huu baada ya kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili tangu Oktoba 25 mwaka jana baada ya kuvunjika mkono wa kushoto kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

Kabla ya kupata majeraha hayo dube alikuwa tayari amehusika kwenye mabao kumi ya Azam kwenye Ligi Kuu Bara akifunga mabao sita na kuasisti mara mbili,

Akizungumzia maendeleo ya nyota huyo baada ya kurejea uwanjani, kocha msaidizi wa Azam, Vivier Bahati amesema: “Prince Dube ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi chetu, mwanzoni mwa msimu huu aliongoza msimamo wa wafungaji ambapo mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao sita kwenye ligi.

“Kwa bahati mbaya mwishoni mwa mzunguko wa kwanza alipata majeraha baada ya kuvunjika mkono kwenye mchezo dhidi ya Yanga na tangu hapo ameonekana kupunguza hali ya kujiamini.

“Hivyo kama benchi la ufundi tumeamua kumlinda kwa kumpa programu za tofauti na ilivyokuwa mwanzo, kwa mfano kwa sasa tumempunguzia majukumu ya kushambulia wakati wa kona ambapo inapotokea mipira kama hiyo tumemwambia yeye acheze mipira ya pili ‘Second Ball’ kwa kutokea pembeni,”

SOMA NA HII  AZAM FC YAWAPA TANO WACHEZAJI WAKE KUITWA STARS