Home kimataifa CHELSEA NA LIVERPOOL ZAVURUGWA, KISA DAYOT

CHELSEA NA LIVERPOOL ZAVURUGWA, KISA DAYOT


MABOSI wa Bayern Munich wamethibitisha kuwa wamefikia makubaliano mazuri na Klabu ya RB Leipzig kupata saini ya nyota wao Dayot Upamecano kwa dau la pauni milioni 38.5.

Nyota huyo mwenye miaka 22 anatajwa kuwa pia kwenye rada za Liverpool na Chelsea ambao wamekuwa wakipambana kuisaka saini ya beki huyo raia wa Ufaransa.

Suala hilo linatajwa kuwavuruga vigogo wa Ligi Kuu England ambao walikuwa wanahitaji saini yake kwa ajili ya msimu ujao.

Mabosi hao wa Bayern Munich wameeleza kuwa wamefikia makubaliano ya kumpa dili la miaka mitano beki huyo ili aweze kujiunga na timu hiyo ambayo imetwaa taji la Klabu Bingwa Duniani.

Kiongozi wa Bayern Munich, Hasan Salihamidzic amesema kuwa wamekuwa kwenye mazungumzo mazuri na wakala wa mchezaji huyo Volker Struth kwa muda mrefu jambo ambalo linawafanya waamini kwamba watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kumpata mchezaji huyo.

“Amekubali kupewa saini ya miaka mitano hivyo dili hilo litamfanya awe ndani ya Uwanja wa Allianz Arena msimu ujao.Tumekuwa na mazungumzo mazuri na tunaamini kwamba tumezungumza naye na kumpa kile ambacho tunakihitaji.

“Tunaamini kwamba kuna ushindani mkubwa na yeye pia ni mchezaji mzuri mwenye uwezo ndani ya uwanja hasa ukizingatia kwamba ana umri wa miaka 22,”


SOMA NA HII  ARSENAL KUMTOA LACAZETTE