Home Simba SC KOCHA SIMBA AWAANDALIA AS VITA SAPRAIZI

KOCHA SIMBA AWAANDALIA AS VITA SAPRAIZI


KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes amejiandaa kuwasapraizi wapinzani wao AS Vita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na AS Vita ya DR Congo, kwa kuwapa nafasi baadhi ya nyota ambao hawakuonekana katika michezo yao iliyopita.

Mchezo huo wa kwanza wa kundi A, unatarajiwa kupigwa katika dimba la Martyrs, uliopo Kinshasa nchini Congo majira ya saa 11 jioni kwa saa za DR Congo ambayo ni sawa na saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Simba iliondoka jana saa 10 jioni uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar ikiwa na wachezaji wake wote mahiri akiwemo kiungo Jonas Mkude na tayari wameshatua jijjini Kinshasa,Congo.

Akizungumzia mipango yao kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes Da Rosa amesema: “Tumejiandaa vizuri na mchezo wetu wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya AS Vita, tunajua hautakuwa mchezo rahisi kutokana na ubora wa wapinzani, lakini tumejipanga kukabiliana na hali hiyo ili kuweza kupata ushindi katika mchezo huo.

“Kuelekea mchezo huo tutakuwa na sapraizi ndani ya kikosi chetu, ambapo kutakuwa na mabadiliko ya baadhi ya wachezaji ambao hawakucheza michezo iliyopita.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIONA SIMBA INAVYOCHEZA JANA ....MCHAMBUZI NGULI AMSHUKIA KOCHA MAKI...AMPA ONYO LA YANGA...