Home kimataifa LIVERPOOL YAPIGWA MARUFUKU KUKANYAGA UJERUMANI

LIVERPOOL YAPIGWA MARUFUKU KUKANYAGA UJERUMANI

 

MABINGWA wa England klabu ya Liverpool, haitaruhusiwa kuingia nchini Ujerumani kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya RB Leipzig, kutokana na vizuizi vilivyowekwa na taifa la Ujermani kwa wageni kutoka England ikiwa ni hatua za kujikinga na Covid 19.

Wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani imeiarifu klabu ya RB Leipzig kuwa mchezo dhidi ya Liverpool haujakidhi mahitaji kulingana na kanuni za sasa za kujikinga na virusi vya Corona, mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa klabu bingwa ulaya hatua ya 16 bora umepangwa kuchezwa Februari 16, 2021.

Taifa la Ujerumani limeweka vizuizi kwa baadhi ya wasafiri kuingia nchini humo kutoka kwenye mataifa ambayo yanamaambukizi ya juu ya virusi vya Corona, ambapo England ni moja ya taifa ambalo lipo kwenye orodha hiyo.

Shirikisho la soka barani ulaya UEFA liliboresha kanuni zake juu ya janga la Corona, iliweka wazi kuwa kama timu mwenyeji haiwezi kuandaa mchezo kwenye uwanja wake basi inalazimika kutafuta uwanja mwingine ambao watautumia kuandaa michezo yao ya nyumbani, na kama watashindwa basi timu pinzania itapewa alama 3 na ushindi wa mabao 3-0.

Inaripotiwa kuwa uwanja wa Puskas uliopo mjini Budapest nchini Hangary ndio utakao tumika kuandaa mchezo huo kama uwanja wa nyumbani wa Leipzig lakini pia inatajwa mchezo huo unaweza kufanyika kwenye moja ya viwanja nchini England.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPIGIKA SANA ....MAN UTD WAFUFUKIA MBELE YA LIVERPOOL....'UZEE' WAMPONZA RONALDO....