Home Azam FC MTAMBO WA MABAO AZAM FC WAJA TOFAUTI NA KAGERE,ADAM

MTAMBO WA MABAO AZAM FC WAJA TOFAUTI NA KAGERE,ADAM


 PRINCE Dube, nyota wa Azam FC ambaye ni mtambo namba moja wa kutengeneza mabao kwenye kikosi hicho ameamua kuja na muonekano mpya kwa mzunguko wa pili baada ya kuondoa nywele zote kichwani na kubaki na upara.


Azam FC ikiwa imetupia jumla ya mabao 27 amehusika kwenye mabao 11, amefunga mabao 6 na ana pasi 5 za mabao akiwa ni namba moja kwa kikosi hicho ambacho kesho kitamenyana na Mbeya City, Uwanja wa Azam Complex.

Awali nyota huyo alikuwa amenyoa kwa mtindo ule wa panki ambapo alikuwa na  nywele ndefu kimtindo sawa na mshikaji wake Idd Seleman,’Nado’ Yahay Zayd, Nivere Tigere, Ayoub Lyanga hivyo amebadili muonekano na kuungana na staa mwenzake Bruce Kagwa.

Kwa wakali wa kucheka na nyavu ambao ni Meddie Kagere mwenye mabao 9, John Bocco mwenye mabao 8 wote wa Simba, Meshack Abraham wa Gwambina na Adam Adam wa JKT Tanzania wenye mabao saba hakuna mwenye para hivyo Dube anakuja na muonekano wa kipekee kwa wakali wa kutupia.

SOMA NA HII  HUKO LIGI KUU MAMBO NI MOTO, SIO SIMBA, YANGA WALA AZAM, MWAMBA HUYU HAPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here