Home Simba SC MUGALU : HUWA NAWAFUNGA AS VITA KILA NAPOKUTANA NAO..!!

MUGALU : HUWA NAWAFUNGA AS VITA KILA NAPOKUTANA NAO..!!


Kinshasa
. Mshambuliaji wa Simba, Chriss Mugalu ameifungia timu yake bao pekee katika mechi ya mzunguko wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika ilipocheza ugenini dhidi ya AS Vita.

Mugalu alisema juzi kuwa ameifungia timu hiyo kwa mara ya tatu kutokana na sababu mbili kubwa.

Nyota huyo alisema kwanza kocha wa timu hiyo, Frolent Ibenge ndiyo kocha mkuu wa DR Congo ambayo tangu ameanza kazi ya kuifundisha timu hiyo hajawahi kumuita.

“Ndiyo maana kila nikikutana nae huwa napambana kuliko kawaida ili kumuonyesha ninao uwezo wa kuitwa katika timu hiyo na nikafanya vizuri kama ambavyo nafanya katika klabu.

“Najua mara zote nikimuonyesha uwezo ambavyo nacheza na kumfunga huwa haniiti, ila kwa ambavyo nimeonyesha kiwango bora katika mechi hii sioni tena sababu ya kuniacha.

“Jambo la pili nilijituma na kucheza zaidi kutokanakuwa katika ardhi ya nyumbani kwetu, ambayo natakiwa kuonyesha nipo katika kiwango bora zaidi ya mara ya mwisho walipo niona.

“ Nashukuru Mungu hilo nililisema pia juzi na nikaenda kulitimiza kwa matendo pale uwanjani, kikubwa nimefurahi kuipata timu yangu ushindi muhimu katika mechi hiyo.

“Wakati nacheza FC Lupopo ya hapa nyumbani niliwafunga AS Vita mara moja, lakini nilipokwenda Zambia nilikuja hapa nikawafunga na wakati huu nipo na Simba nimewafunga tena,” alisema.

Katika hatua nyingine Mugalu alisema katika maisha yake ya soka huwa na uwezo mkubwa wa kufunga mabao mengi mara kwa mara katika kila timu ambayo anacheza.

“Kama akili yangu inakuwa sawa na kutulia bila changamoto ya aina yoyote huwa nafunga mabao mengi na mara kwa mara,” aliongeza.

SOMA NA HII  SAA MOJA KABLA YA KUSHUKA DIMBANI..SIMBA WAPEWA MCHONGO WA KUIUA BERKANE...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here