Home news NAMUNGO FC KUANZA SAFARI KURUDI BONGO LEO

NAMUNGO FC KUANZA SAFARI KURUDI BONGO LEO


 BAADA ya kikosi cha Namungo FC kukwama Angola ambapo kilikwenda kwa ajili ya kushiriki mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya 1 de Agosto, leo wanatarajia kuanza safari ya kurudi Bongo.

Kikosi hicho kilizuiwa Uwanja wa Ndege Angola kwa maelezo kwamba kuna wachezaji watatu na kiongozi mmoja wamekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona. 

Mwenyekiti wa Namungo FC, Hassan Zidadu amesema kuwa wamenyanyaswa bila sababu za msingi kwa kuwa sababu za kuzuiwa kwao ni za uongo mtupu.

“Tumezuiwa bila sababu na tumenyanywaswa kwa kuwa walitaka tuwaache wenzentu wanne na sehemu ambayo walipelekwa haikuwa salama kwa kuwa hakukuwa na huduma yoyote ambayo wamepewa.

“Wametuambia kwamba walikuwa wamewapima mara mbili ila sisi tulipoongea nao wamesema hawajapimwa tena, katika hili hatuna amani tunahitaji kurudi Tanzania kwa amani, mtuombee Watanzania ili turudi salama,”.

Jana kilikwama kuanza safari kwa kuwa mamlaka ya Angola ilitaka watu hao wanne waachwe karantini jambo ambalo hawakukubaliana nalo.

Baada ya mambo kukaa sawa leo Februari 15 wanatarajia kurudi Tanzania huku wakisubiri maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Afrika,(Caf) kuhusu mchezo huo ambao ulipaswa kuchezwa Februari 14.

Mchezo huo ulifutwa na Caf wenyewe baada ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kufuatilia suala hilo ambalo limekuwa kwenye mazingira ya hujuma kwa kivuli cha Corona.

Wachezaji wake wanne na kiongozi mmoja watabaki karantini nchini Angola kwa kuwa hawajaruhusiwa kutoka na mamlaka ya Angola.


SOMA NA HII  RASMI:- TANZANIA KUANDAA MASHINDANO YA CHAN 2024...CAF WATIA BARAKA....