Home Simba SC NYOTA YANGA AMPA TANO MZAMIRU YASIN,CHEKI REKODI ZAKE

NYOTA YANGA AMPA TANO MZAMIRU YASIN,CHEKI REKODI ZAKE


  
ALLY Mayayi, nyota wa zamani wa kikosi cha Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa miongoni mwa viungo wazawa ambao wanafanya kazi yao kwa umakini ni pamoja na Mzamiru Yassin.


Yassin alikuwa miongoni mwa wachezaji walioanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ambapo walianza pamoja na Thadeo Lwanga.

Mayayi amesema kuwa uwezo wa kuzuia na kukaba unazidi kuimarika kwa nyota huyo hivyo ni jukumu lake kulinda uwezo wake ili kuendelea kuzifukuzia ndoto za timu.

“Ninaona kwamba moja ya sehemu ambayo Gomes,(Didier) alifanikiwa ni kuwatumia wale viungo wakabaji wawili Lwanga,(Thadeo) na Mzamiru,(Yassin) ila ninaona kwamba taratibu Mzamiru anazidi kuwa bora zaidi kila iitwapo leo hivyo jukumu lake ni kulinda ubora wake,” amesema.

Ndani ya Ligi Kuu Bara, Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 17 nyota huyo amecheza jumla ya mechi 13 na amekosekana kwenye mechi nne. Ametupia mabao mawili kati ya 41.

Jumla ametumia dakika 713 na mechi zake ilikuwa namna hii:-Ihefu, 90,Mtibwa Sugar dk 77,Biashara United dk 90,Gwambina dk 90,JKT Tanzania dk 31, Prisons dk 17,Ruvu Shooting dk 57, Kagera Sugar dk 13,Yanga dk 85,Polisi Tanzania dk 82,KMC 57,Dodoma Jiji 20 na Azam FC 4.

SOMA NA HII  SIMBA WAONA ISIWE TABU YAWARUHUSU MASTAA WAKE KUTUA HUKU