Home Simba SC SIMBA KUREJEA KAMBINI KESHO

SIMBA KUREJEA KAMBINI KESHO


 BAADA ya jana Januari 31 kufanikiwa kutwaa taji la Kwanza ndani ya 2021, Mabingwa wa Ligi Kuu Bara,  Simba wanatarajia kurejea kambini kesho Februari 2 kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara. 


Simba ilishinda taji la Simba Super Cup lililoanza Januari 27 na lilishirikisha timu tatu ambapo wenyeji Simba, Al Hilal na TP Mazembe. 


Mchezo wa mwanzo Januari 27, Simba ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal ambao walishinda wao mbele ya TP Mazembe,  Januari 29 kwa mabao 2-1 hivyo wakawa washindi wa pili.


TP Mazembe ililazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Simba, jana Januri 31 hivyo wakawa washindi wa tatu na pointi yao ni moja huku Simba ikiwa na pointi nne.


Haji Manara,  Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa leo wachezaji wamepewa mapumziko ila kesho watarejea kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, Februari 4, Uwanja wa Jamhuri Dodoma.


“Baada ya kumaliza mashindano ya Simba Super Cup wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja hivyo kesho watarejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi.


“Mashabiki pamoja na timu ambazo zimeshiriki  zinahitaji pongezi kwa kuwa zilikuwa pamoja nasi na mashabiki wameshuhudia burudani hivyo tunasema asante,changamoto zilizotokea tunazifanyia kazi,”.

SOMA NA HII  WAWILI WA SIMBA KUIKOSA YANGA KESHO KWA MKAPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here