Home Simba SC SIMBA YAPANIA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA

SIMBA YAPANIA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA

 


BEKI mkongwe ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, Shomari Kapombe amesema kuwa wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye hatua za kimataifa kutokana na wachezaji kuwa na morali wa kusaka ushindi ndani ya uwanja.

 Simba ipo kundi A hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ipo kundi moja na Al Ahly ya Misri,Al Merrik ya Sudan na AS Vita ya Congo.

Mchezo wake wa kwanza kimataifa ilishinda bao 1-0 dhidi ya AS Vita, Februari 13, nchini Congo ina kibarua cha kuvaana na Al Ahly ya Misri Februari 23, Uwanja wa Mkapa.

 Akizungumza na Spoti Xtra, Kapombe alisema kuwa kila siku wamekuwa wakikumbushana kuhusu malengo yao kimataifa jambo ambalo linawapa nguvu ya kuzidi kupambana.

“Kila wakati tunapokuwa pamoja kambini, mazoezini tunakumbushana kuhusu malengo ya timu hivyo jambo hilo linatupa nguvu ya kufanya vizuri kimataifa, mashabiki watupe sapoti tuna amini tutafikia malengo yetu,” alisema.

Kapombe ni chaguo la kwanza la Gomes pia hata zama za Sven Vandenbroeck ambaye kwa sasa yupo na Klabu ya FAR Rabat alikuwa chaguo la kwanza na alicheza mechi zote za kimataifa ikiwa ni pamoja na ile ya Plateau United ya Nigeria na FC Platinum ya Zambia.

SOMA NA HII  FT:SIMBA 3-0 COASTAL UNION....'KOMBINESHENI' YA CHAMA NA MIQUISSONE MHH...!!