Home Simba SC TUISILA KISINDA AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUIBUKIA NDANI YA SIMBA

TUISILA KISINDA AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUIBUKIA NDANI YA SIMBA


 TUISILA Kisinda, nyota wa kikosi cha Yanga amesema kuwa hana mpango wa kucheza ndani ya Simba kwa kuwa maisha yake kwa sasa yanaendelea vizuri ndani ya mtaa wa Jangwani.

Nyota huyo ambaye ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze ni miongoni mwa viungo ambao wanafanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kulikuwa na habari kwamba miongoni mwa nyota ambao wanahitajika ndani ya Simba ni pamoja na Kisinda jambo ambalo nyota huyo ameligomea.

“Kwa sasa bado nipo ndani ya Yanga na sina mpango wa kuondoka hivyo mashabiki wasiwe na mashaka sifikirii kwenda Simba.

“Maisha yetu ndani ya kikosi ni mazuri na kila mmoja anafurahi kile ambacho anakifanya hivyo ni wakati wetu wa kuendelea kufanya vizuri,” .

Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa imekusanya jumla ya pointi 44,imecheza mechi 18 bila kupoteza huku ikiwa imeshinda mechi 13 na ina sare 5.

SOMA NA HII  MABOSI SIMBA WAANZA NA HUYU