Home kimataifa WINGA SANCHO AWEKA REKODI YAKE YA KUCHEKA NA NYAVU

WINGA SANCHO AWEKA REKODI YAKE YA KUCHEKA NA NYAVU


 WINGA wa Klabu ya Borrusia Dortmund, Jadon Sancho ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kufikisha jumla ya mabao 35 ndani ya Bundesliga.

Winga huyo mwenye miaka 20 anatajwa kuingia anga za Manchester United amekuwa kwenye ubora tangu alipoibuka ndani ya Dortmund msimu wa 2017 akitokea Klabu ya Manchester City.

Mbali na nyota huyo kufaya hivyo pia mshambuliaji wa kikosi cha timu hiyo Erling Haalad naye yupo mbioni kuweka rekodi ya namna hiyo kwa kuwa ametupia jumla ya mabao 30 ndani ya Bundesliga.

Sancho msimu huu ametupia jumla ya mabao matano na kutoa pasi nane huku Haalad yeye akiwa amefunga mabao 17 katika mechi 17 za Bundesliga.

Habari zinaeleza kuwa Kocha Mkuu wa United, Ole Gunnar Solkjaer anamtazama kwa ukaribu nyota huyo ili aweze kupata saini yake.

SOMA NA HII  MABOSI WA DORTMUND WAWEKA UGUMU USAJILI WA HAALAD