Home Ligi Kuu YUSUPH MHILU:MZUNGUKO WA PILI TUTAPAMBANA KUFANYA VIZURI

YUSUPH MHILU:MZUNGUKO WA PILI TUTAPAMBANA KUFANYA VIZURI


YUSUPH Mhilu, nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars anayecheza ndani ya Kagera Sugar amesema kuwa wamekubaliana kupambana ndani ya uwanja kupata pointi tatu kwenye mechi zao za mzunguko wa pili.

Mhilu ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Stars kilichoshiriki Chan, nchini Cameroon ndani ya ligi ametupia jumla ya mabao matano na pasi moja ya bao kati ya mabao 19 yalifungwa na timu yake iliyo nafasi ya 9 kwenye msimamo.

Bao lake la tano alitupia Uwanja wa Kaitaba wakati timu yake ikigawana pointi mojamoja na Gwambina FC.

 Mhilu amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya ndani ya uwanja hasa ukizingatia kwamba ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi.

“Bado ushindani ni mkubwa ndani ya uwanja hilo linatufanya nasi tujipange kufanya vizuri hasa mzunguko huu wa pili. Kwetu sisi kila mechi tunaamini tutafanya vizuri.

“Kugawana pointi moja na Gwambina ilituumiza ila kwa kuwa ni sehemu ya matokeo tutajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo ndani ya ligi,”.  

Mchezo ujao wa Kagera Sugar unatarajiwa kuwa dhidi ya Yanga utaokachezwa Uwanja wa Mkapa.  

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA HUU HAPA