Home Azam FC AZAM FC V IHEFU TAMBO KAMA ZOTE

AZAM FC V IHEFU TAMBO KAMA ZOTE

 


LEO Machi 11, Uwanja wa Azam Complex miguu ya wanaume 22 itakuwa kazini kuzisaka pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.


George Lwandamina,  Kocha Mkuu wa Azam FC ana kibarua cha kuzuia ngome yake inayolindwa na kipa namba moja Mathias Kigonya huku Zuber Katwila akimuamini kijana wake Deogratius Munish.


Mchezo wa mzunguko wa kwanza ambapo ilikuwa ni kete ya kwanza kwa Katwila alishuhudua vijana wake wakikubali kuokota nyavuni mabao mawili na kuacha pointi tatu mazima zikisepa.


Watupiaji wa mabao kwa Azam FC ni Idd Seleman, ‘Nado’ na Ayoub Lyanga ambapo mpishi wa mabao hayo alikuwa  ni mwana wa mfalme, Prince Dube ila leo atakosekana kwa kuwa anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja.


Lwandamina amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na wanahitaji pointi tatu muhimu hivyo watapambana. 


Katwila amesema kuwa kila mchezo kwao wanahitaji pointi tatu ili waweze kubaki ndani ya ligi msimu ujao.


Ihefu ipo nafasi ya 16 na pointi zake ni 20  inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya 3 na pointi zake ni 41.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA 2020/21 UPO NAMNA HII