Home Simba SC BEKI MKONGO: NI KWELI SIMBA WAMENIFUATA

BEKI MKONGO: NI KWELI SIMBA WAMENIFUATA


BEKI wa kulia wa AS Vita, Shabani Djuma amekiri kuwa ni kweli alifuatwa na viongozi wa Simba ili kuangalia uwezekano wa kujiunga nao mwishoni mwa msimu.

Djuma amekuwa katika kiwango bora ndani ya AS Vita ambapo msimu huu katika michuano yote aliyoichezea timu hiyo amefunga mabao 6 na kutoa pasi tano za mabao.

Akizungumzia uwezekano wa kutua Simba Djuma amesema: “Ni kweli kuna baadhi ya viongozi wa Simba walinitafuta kwa ajili ya mzungumzo ya awali ya usajili lakini siwezi kulizungumzia sana hilo kwani sasa.

“Hii ni kwa sababu wote kwa sasa tunapambana kuzisaidia timu zetu zifanye vizuri katika michuano ya kimataifam ikizingatiwa tupo kundi moja.

Kutokana na uwezo wa beki huyo, ni wazi endapo beki atafanikiwa kujiunga na Simba ataenda kugombea namba na Shomari Kapombe ambapo utakuwa mtihani mgumu kwa kocha kuchagua nani wa kuanza kulingana na ubora wa mabeki hawa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF DHIDI YA USGN..SIMBA WAONA ISIWE TABU..YAWACHIA UBINGWA YANGA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here