Home Ligi Kuu MKWASA ATAJA KILICHOIPOTEZA RUVU SHOOTING

MKWASA ATAJA KILICHOIPOTEZA RUVU SHOOTING


KOCHA mkuu wa klabu ya Ruvu Shooting, Charles Boniface Mkwasa ameweka wazi kuwa, sababu kubwa ya kutokuwa na matokeo mazuri katika michezo yao ya hivi karibuni ni kujiamini kulikopitiliza kwa wachezaji wake kiasi cha kufanya makosa mengi.

Ruvu Shooting imeshinda mchezo mmoja pekee kati ya michezo minne iliyopita ya Ligi Kuu waliyocheza huku pia wakikubali kupoteza michezo mitatu iliyosalia.

Kutokana na matokeo hayo Ruvu imeporomoka kutoka nafasi ya nne ya msimamo waliyotawala kwa muda mrefu, mpaka nafasi ya sita baada ya kujikusanyia pointi 34 kwenye michezo 24 waliyocheza mpaka sasa.

Akizungumzia hali hiyo, Ofisa habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema: “Baada ya kusimama kwa muda kwa ligi ili kupisha michuano ya kimataifa, tuliwapa mapumziko mafupi nyota wa kikosi chetu na kufanya kikao na benchi la ufundi ili kutathimini juu ya mwenendo wetu usioridhisha katika siku za hivi karibuni.

“Kocha akatuweka wazi kuwa miongoni mwa changamoto ambazo wachezaji wetu walikuwa nazo ni kujiamini kulikopitiliza, na kukosa umakini kiasi cha kushindwa kutumia nafasi nyingi za wazi ambazo tuliweza kutengeneza.

“Lakini hali hii pia iliathiri uthabiti wetu wa kuzuia, jambo ambalo limeanza kufanyiwa kazi baada ya timu kurejea kambini Jumanne ya wiki iliyopita,”

SOMA NA HII  MKANDALA ATUMA UJUMBE HUU KWA SIMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here