Home Simba SC MONALISA AANZA NA MIKWARA SIMBA QUEENS

MONALISA AANZA NA MIKWARA SIMBA QUEENS

 BAADA ya klabu ya Simba Queens, leo kumtambulisha rasmi muigizaji, Yvonne Cherrie maarufu ‘Monalisa’ kuwa msemaji wa kikosi hicho, tayari msemaji huyo ameanza mikwara ya hatari.

Monalisa amekaribishwa rasmi ndani ya Simba Queens na mlezi wa klabu hiyo, Fatema Dewji.

Akizungumza baada ya uteuzi huo Monalisa alisema: “Mimi ni Simba jike (Simba Queen), ahsante Mungu, ahsante wanasimba wote na mwisho Ahsante mama mlezi wa Simba Queens, Fatema Dewji kwa kunikabidhi kijiti cha kuisemea Timu yangu pendwa.

“Sasa ni muda wa kazi, muda wa kuionesha dunia ukubwa wa Simba, mwisho naomba kutoa tangazo rasmi ya kwamba kila binti/Mwanamke nchi hii ni shabiki wa Simba Queens,”

SOMA NA HII  BOSI SIMBA AFUNGUKA MBRAZILI KUPIGWA CHINI...."TIMU TUNAYOITAKA BADO SANA"...