Home Yanga SC MTAMBO WA MABAO YANGA WAOMBA SAPOTI YA MASHABIKI, WAAHIDI KUPAMBANA

MTAMBO WA MABAO YANGA WAOMBA SAPOTI YA MASHABIKI, WAAHIDI KUPAMBANA

 MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga, Deus Kaseke amesema kuwa watazidi kupambana ndani ya uwanja ili kupata matokeo chanya kila wakati.

Yanga imetoka kumalizana na Ken Gold inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Katika mchezo huo Yanga ilishinda bao 1-0 na kuwafanya watinge hatua ya 16 bora huku nyota wao Carlos Carlinhos akionyeshwa kadi ya nyekundu ya moja kwa moja baada ya kuonekana akimpiga ngumi beki wa Ken Gold,  Boniphace Mwanjonde dakika ya 80.

Ndani ya ligi Yanga ikiwa imetupia jumla ya mabao 34 amehusika kwenye mabao 7, akiwa amefunga mabao sita na kutengeneza nafasi moja ya bao uwanjani.

Kesho, Machi 4 Yanga ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union ambapo Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza , Uwanja wa Mkapa Yanga ilishinda mabao 3-0.

Kaseke amesema:”Ushindani ni mkubwa nasi pia tunajua hilo kikubwa ni mashabiki kuendelea kutupa sapoti ili tufanye vema ndani ya uwanja na kila kitu kinawezekana, sisi tutazidi kupambana ili kupata matokeo mazuri, ” .

Kwenye msimamo, Yanga ipo nafasi ya kwanza na ina pointi 49 baada ya kucheza jumla ya mechi 21 inakutana na Coastal Union iliyo nafasi ya 13 na pointi 23.

SOMA NA HII  KUELEKEA USAJILI DIRISHA DOGO...MAKUSU AZICHONGANISHA SIMBA NA YANGA...AZIITA TENA....